Ligi ya Premia ya Uingereza kuanza Kesho
Huwezi kusikiliza tena

Ligi ya Premia ya Uingereza kuanza Kesho

Hatimaye kiu cha mashabiki wa soka hususan Ligi kuu ya Uingereza kitaanza kukatwa wikendi hii pale ligi hiyo maarufu ya EPL, itakapoanza rasmi kutimua kivumbi katika msimu huu wa 2014/2015.

Huu ni wakati ambao kwa wale mashabiki wa soka hasa wa timu kubwa Liverpool,Manchester United ,Arsenal,Chelsea na Man City watakapokuwa matumbo joto kwa kufuatilia mechi zinazohusu timu zao.