Huwezi kusikiliza tena

Canada yatoa Chanjo ya Ebola

Canada imesema itatoa dozi 1,000 za chanjo ya majaribio ya Ebola ili kusaidia kupigana na mlipuko wa ugonjwa huo Afrika magharibi.

Hii ni baada ya shirika la afya duniani WHO kuidhinisha matumizi ya dawa ambazo hazijakamilishwa majaribio ilikuokoa maisha ya watu walioambukizwa Ebola.

Licha ya hayo wataalamu wanasema usambazaji wa dawa hiyo ya Zmapp ni mdogo sana kwani inagharimu muda mrefu kwa wanasayanzi kukuza mimea inayotoa dawa hiyo kwa wingi .

Zaidi ya watu 1,000 wamekufa kutokana na mlipuko huu wa majuzi magharibi mwa Afrika.