Familia yawachwa hoi baada ya kupigwa risasi kwa watoto pwani
Huwezi kusikiliza tena

Kijana mwenye miaka 4 akatwa mguu Kenya

Polisi nchini Kenya wamelaumiwa kwa kumpiga risasi kijana mmoja mwenye umri wa miaka 4 aliyepigwa risasi katika hali ya kutatanisha wakati wa mauaji ya mfanyibiashara Shahid Butt huko Mombasa mwezi uliopita.

Mtoto huyo sasa amekatwa mguu wake .

Familia ya mvulana huyo inasema kwamba serikali imewatelekeza licha ya kutoa ahadi chungu nzima.

Mwandishi wa BBC John Nene alitembelea famila yake na kutuandalia taarifa ifuatayo.