Huwezi kusikiliza tena

Ebola:Daktari aaga Nigeria

Serikali ya Nigeria imethibitisha kutokea kifo cha daktari mmoja kutokana na ugonjwa wa Ebola katika mji wa Port Harcout nje ya mji wa Lagos.

Watu wengine zaidi ya sabini wanachunguzwa mjini humo huku mke wa daktari huyo akiwekwa katika chumba chake kando kufanyiwa uchuguzi zaidi.

Daktari huyo alimtibu mgonjwa wa Ebola ambaye alifanikiwa kupona. Mwanamume huyo inaarifiwa alikutana na Patrick Sawyer, mwanamume aliyeeneza Ebola kutoka Liberia hadi Nigeria.