Huwezi kusikiliza tena

Ufisadi unaua mamilioni duniani

Inakisiwa dola Trilloni 1 huporwa kutoka kwa nchi maskini kila mwaka huku maisha ya mamilioni ya watu katika nchi hizo yakihatarishwa.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kupambana na umaskini la 'Organisation one'.

Shirika hilo linasema kwamba faida zilizofikiwa katika kupambana na umaskini katika miongo miwili iliyopita, zinakabiliwa na tisho kubwa kwa sababu ya viwango vya juu vya ufisadi na uhalifu.

Matukio ya ufisadi ni pamoja na utumiaji wa makampuni ghushi na utengezaji wa pesa kwa njia haramu.