Huwezi kusikiliza tena

Polisi wakana mauaji migodini TZ

Polisi nchini Tanzania wamekanusha madai ya ukiukaji haki za binadamu pamoja na mauaji dhidi ya wakazi wa eneo la Nyamongo linalozunguka mgodi wa machimbo ya dhahabu wa North Mara Wilayani Tarime mkoani Mara.

Hii inatokana na manung'uniko ya wakazi wa eneo hilo, kwamba polisi mara kwa mara wamevishambulia vijiji hivyo kwa kuwapiga watu wakiwemo kina mama wajawazito, na kusababisha majeraha na hata vifo.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau alitembelea Nyamongo.