Tahadhari kwa wanaume Kenya

Tahadhari kwa wanaume Kenya

Tahadhari kwa wanaume wanaowatelekeza watoto wao nchini Kenya.Baadhi tayari wameanza kupata tumbo joto.

Kikundi cha wanaume watatu nchini Kenya kimezindua ukurasa wa Facebook ambao lengo lake ni kuwajibisha wanaume wasiotekeleza majukumu yao ya kuwalea watoto wao.Mtandao huo unaitwa Deadbeat Kenya.

Mtandao huo tayari umepata mashabiki wengi sana huku baadhi ya wale walioaibishwa wekiwemo wanasiasa, wanamuziki na watu mashuhuri.

Kwa nini mwanamume mwenye uwezo amtyelekeze mtoto wake? Baadhi ya wanaume wanalalamika kuwa wanawake ni wajanja kwani wanashika mimba kwa njia za kijanja.

Na je Jackson Njeru mwanamume aliyeanzisha ukurasa huu wa Facebook hahofii maisha yake? Hilo ni moja ya maswali aliyoulizwa na mwandishi wa BBC Dayo Yusuf