Kwa nini Scotland inataka kujitenga?

Kwa nini Scotland inataka kujitenga?

Alhamsi wananchi wa Scotalnd watapiga kura ya maamuzi ikiwa wajitenge na Uingereza au la. Wananchi watajua ikiwa Scotland itajiondoa kutoka muungano na Uingereza, muungano ambao umedumu kwa miaka 307.

Duru zinasema kuwa kura ya maoni inaonyesha kuwa kuna ushindani mkubwa kati ya wanaotaka muungano kuvunjwa na wale wanaotaka muungano kusalia.

Zaidi ya wafanyabiashara 130 walitia saini barua ya kutaka muungano kutovunjika wakati wafanyabiasha wengine 200 wakitaka Scotland ijitenge.