Sauti ya ninga yawatetea wakimbizi

Aziza Brahim ni mwanamuzikiambaye ni mjumuu wa Al Khadra, gwiji wa mashahiri ya Sahrawi .

Wengi wanasema sauti yake inamtoa Nyoka pangoni na sasa anajulikana kama mmoja wa wanamuziki mashuhuri Magharibi mwa jangwa la Sahara.

Aziza alizaliwa na kulelewa katika kambi za wakimbizi za Saharawi Kusini Magharibi mwa Algeria lakini maisha halisi ya kambini ndiyo yaliyomfanya kwenda kusomea nchini Cuba na sasa anaishi ndhini Barcelona.

Aziza hunchanganya mziki wa kitamaduni na nyimbo za Blues pamoja na za kihispania.

Zaidi yeye huzungumzia matatizo yanayotokana na kuwa mkimbizi.

Album yake 'Soutak' ilitoka mapema mwaka huu.