Mahasimu walivyopepetana Scotland

Kabla ya uamuzi wa kujitega na au kusalia Uingereza, waskochi walifanya kampeini zenye hekaheka kubwa kila mwambangoma akivuta kwake.

Waziri kiongozi wa Uskochi, Alex Salmond, aliendelea kuwahakikishia wapigaji kura wataendelea kutumia sarafu ya pauni, hata kama wataamua kujitenga.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown, naye aliwataka wapigaji kura kukataa kile alichokiita uzalendo hafifu, na kuonya uchumi wa Uskochi huenda ukazorota.

Peter Musembi anaarifu zaidi kutoka Glasgow.