Ebola:Mafanikio yapatikana Sierra Leone

Serikali ya Sierra Leone ilitangaza amri ya siku tatu ya kutotoka nje ikilenga kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

Imetangaza mafanikio makubwa kwani ugonjwa umeweza kudhibitiwa huku wagonjwa zaidi wakipatikana na wengine wakichunguzwa, kubaini ikiwa wanaugua Ebola.

Hata hivyo baadhi ya wataalamu wa afya wamekosoa amri hiyo wakisema itaharibu ushirikiano uliopo kati ya wagonjwa na madaktari.

Sierra Leone ni moja ya nchi zilizoathirika zaidi kutokana na Ebola huku watu 550 wakipoteza maisha yao.