Shambulizi lililotikisa Kenya zaidi

Lilikua shambulio hatari zaidi la kigaidi mpaka sasa nchini Kenya.

Jengo lenye maduka kadha ya biashara la WestGate lililojaa wateja lilishambuliwa na watu wenye silaha huku mamia ya watu wakiwa katika starehe za wikendi.

Takriban watu sabini na wawili waliuawa kufuatia siku nne za mvutano.

Shambulio hilo liligeuza sura ya ulinzi nchini Kenya.

Anne Soy anatuarifu zaidi.