Westgate:Maswali mengi hayajapata majibu

Kenya inaadhimisha mwaka mmoja tangu shambulizi la kigaidi la Westgate jijini Nairobi.

Watu sitini na saba waliuwawa na Zaidi ya watu mia mbili kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab.

Maswali mengi yameendelea kuibuka tangu shambulizi hilo ikiwemo, majina ya washambulizi, na fidia kwa waathiriwa.

Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kubuniwa kwa kamati ya uchunguzi lakini mwaka mmoja baadaye ukweli wa operesheni ya Westgate umefikia wapi?

Mwandishi wetu wa BBC anatupa ripoti ifuatayo.