Vikwazo vya kusaka elimu ya juu

Katika mfululizo wa makala zetu za elimu ya juu, leo tunaelekea nchini Tanzania ambapo pamoja na jitihada za serikali ya nchi hiyo kutaka kuongeza idadi ya wasichana wanaochukua masomo ya sayansi kuanzia ngazi ya chini hadi chuo kikuu,changamoto za kufikia lengo hilo zimekuwa nyingi.

Mwandishi wa BBC Arnold Kayanda amezungumza na Dr Cathbert Nahonyo ambaye ni Mtaalamu wa Baionwai na Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye anaeleza hali ilivyo