Je hali imebadilika nchini Kenya?

Kenya inaadhimisha mwaka mmoja tangu shambulio la kigaidi la Westgate jijini Nairobi. Watu sitini na saba waliuwawa na zaidi ya wengine mia mbili walijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na kundi la Al Shabaab.

Maswali mengi yameibuka tangu shambulio hilo ikiwemo, majina ya walioshambulia na fidia kwa waathiriwa.

Rais Kenyatta aliahidi kutaundwa kamati ya uchunguzi, lakini mwaka mmoja baadaye ukweli wa harakati za Westgate umefikia wapi?

Mwandishi wa BBC Dennis Okari anasimulia zaidi.