Mjasiriamali awavutia vijana Kenya

Martha Chumo ana umri wa miaka 20. Yeye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi wa chuo cha Dev School ambacho huwapa mafunzo vijana wenzake.

Ni mradi ambao umemfanya kutambulika ndani na nje ya Kenya.

Ameteuliwa kuwania tuzo ya ANZISHA ambayo hutambua wafanyabiashara wenye umri wa chini ya miaka 22.

Mwandishi wa BBC Gladys Njoroge alizungumza naye.