Kijana anayewafunza wenzake teknolojia

BBC Swahili inaangazia swala kuu la elimu ya juu, huku vyuo vikuu vikishindwa kuhudumia idadi kubwa ya wanafunzi wanaofuzu kujiunga navyo.

Kijana wa kike nchini Kenya anawapa fursa wanafunzi kujifunza maswala ya programu za Komputa.

Martha Chumo mwenye umri wa miaka 20 ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi wa chuo cha Dev School ambacho huwapa wanafunzi mafunzo hayo. Ni mradi ambao umemfanya kutambulika ndani na nje ya Kenya.

Ameteuliwa kuwania tuzo za mwaka huu za ANZISHA ambazo hutambua wafanyabiashara wenye umri wa chini ya miaka 22.

Gladys Njoroge ametembelea shule hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.