Tumi Molekane ni mtunzi na msanii aliyekamilika
Huwezi kusikiliza tena

Tumi anaporomosha mistari kutoka A.Kusini

Msanii mtunzi wa nyimbo na mashairi kutoka Afrika Kusini Tumi Molekane ndiye anayetupambia ukurasa wetu wa Burudani kwa leo.

Licha ya kuwa amejitenga na kundi lake la awali la 'The Volume', Tumi aliungana tena na mpiga gita kutoka Msumbiji Tiago Correia-Paulo ilikunasa kipande hichi cha ngoma yake kwa ajili yako mpendwa unayeitegea BBC.

Ajabu ni kuwa wimbo wake huu ulitokana na mende.

Alikuwa ameketi jikoni akamuona mende mara huyo mende akatoweka ,akajichomeka ndani ya mwanya ilikuepuka dhoruba yake.

Ngoma hii iko katika Album yake Solo ya Rob the Church aliyoitoa Agosti mwaka huu.

Album hii ilifuatia ziara yake katika mataifa mbalimbali Afrika akirekodi filamu kwa jina ''Afrique'' na inamuingiliano wa rap na Afrobeat,,,,Burudika