Huwezi kusikiliza tena

Mo Ibrahim:Mizani ya demokrasia Afrika

Wakfu wa Mo Ibrahim umesema kuwa mizani ya utawala bora katika mataifa matano ya Afrika imeshuka.

Kinachoshangaza ni kuwa mataifa haya yamekuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa zinasifiwa kwa utawala mzuri wa kidemokrasia.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wakfu huo ikitathmini utawala wa kidemokrasia barani Afrika.

Katika miaka mitano iliyopita, mataifa ya Botswana, Cape Verde, Mauritius, Seychelles na Afrika Kusini South Afrika yalishuka daraja moja katika mizani hiyo, iliyoangazia zaidi utawala wa kisheria, haki za kibinadamu, usalama , kuhusishwa kwa wananchi katika maswala ya utawala , uchumi endelevu na nafasi za maendeleo.

Wakfu huo umekuwa ukiwatuza marais wenye sifa nzuri ya kutawala nchi zao kwa njia ya kidemokrasia.

Tangu kuanzishwa kwake na mwekezaji wa Sudan Mo- Ibrahim Miongoni viongozi waliotuzwa ni pamoja marais wa zamani Pedro Verona Pires wa Cape Verde, Festus Mogae kutoka Botswana na Joaquim Chissano wa Msumbiji.

Balozi Agustine Mahiga azungumza na BBC kuhusu ikiwa Afrika imefanikiwa kuboresha uongozi wa Kidemokrasia au la.