Ebola:Watoto wanavyotengwa A.Magharibi

Ebola:Watoto wanavyotengwa A.Magharibi

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takriban watoto elfu tano nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone, wamepoteza mzazi mmoja au wawili kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Shirika la umoja huo la kuwahudumia watoto, UNICEF, linasema kuwa kupata watu wa kuwahudumia watoto hao imekuwa vigumu sana kwa sababu ya unyanyapaa unaotokana na ugonjwa huo.