Huwezi kusikiliza tena

Mbunge wa upinzani rumande TZ

Mbunge mmoja wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA amepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza vigezo vya dhamana mahakamani.

Halima Mdee ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chama hicho pamoja na wenzake wanane, walifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakituhumiwa kufanya maandamano yaliyopigwa marufuku.

Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam Baruan Muhuza amefanya mahojiano na msemaji wa chama hicho Tumaini Makene ambaye kwanza anaelezea kwanini Mbunge huyo amekosa dhamana?