Huwezi kusikiliza tena

Kenya:Mke wa rais atetea watoto

Licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa, mradi wa kampeni ya Beyond Zero wa Bi Margaret Kenyatta mkewe Rais wa Kenya wa kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama waja wazito umepokelewa kwa furaha kwa imani ya kufanikiwa katika kaunti ya Taita Taveta eneo la Pwani.

Kaunti hiyo imekabidhiwa gari lenye kliniki ya matibabu ili kuwafikia watu wa vijijini sehemu ambazo hazina hospitali ama zahanati karibu.

Mwandishi wetu John Nene ametuandalia taarifa ifuatayo: