Huwezi kusikiliza tena

Picha ya mahaba yawachongea polisi TZ

Jeshi la polisi nchini Tanzania limewafukuza kazi maafisa wake watatu kwa kosa la kupiga picha ya aibu na kuiweka kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania Henry Mwaibambe ameiambia BBC kuwa askari hao wamekiuka maadili ya kazi yao pamoja na kulidhalilisha jeshi hilo kwakuwa walipiga picha hiyo wakiwa wamevaa sare za jeshi kinyume na sheria.

Askari hao walikuwa kazini wakati wakipiga picha hiyo ambayo ilipigwa na askari mwenzao ambaye pia amefukuzwa kazi, kama ambavyo kamanda huyo alivyosema kwenye mahojiano na mwandishi wa BBC Baruan Muhuza.