Huwezi kusikiliza tena

Heka heka za uchaguzi Msumbiji

Wapiga kura nchini Msumbiji wanaendelea na shughuli ya kumchagua rais mpya na wabunge.

Chama tawala cha Frelimo ambacho kimekuwa madarakani tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake mwaka wa elfu moja mia tisa na sabini na tano, kinakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa chama hasimu cha Renamo.

Kampeni zilimalizika katika hali ya utulivu na mazingira ya shamrashamra, isipokuwa mjini Napula kaskazini mwa nchi.

Vurugu zilizuka kati ya wafuasi wa chama kinachotawala nchini humo cha FRELIMO na kile cha upinzani cha RENAMO.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaza.

Ripoti zinasema zaidi ya watu ishirini walijeruhiwa, na wengine kadhaa kukakamatwa.

Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza yuko nchini Msumbiji