Huwezi kusikiliza tena

Taarifa mseto kuhusu Ebola

Shirika la afya duniani leo linaongoza mkutano wa kamati yake ya dharura , kutathmini hali ya hivi karibuni kuhusiana na mlipuko wa Ebola .

Mkutano huo unafanyaika wakati ugonjwa huo ukiendelea kuenea katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo Guinea, Sierra Leone na Liberia - ingawa Senegal na Nigeria, ambazo zilikuwa na visa vichache zimetangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

Mkutano huo pia utatathmini hatua za kuwapima watu Ebola mipakanai na kuangalia nman wanavyoweza kuwawekea masharti makali zaidi kwa wanasafiri kutoka maeneo yenye Ebola.