Museveni akana njama ya urithi

Museveni akana njama ya urithi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amepinga tuhuma kuwa anamuandaa mtoto wake kumrithi katika madaraka ya urais wa nchi hiyo wakati atakapostaafu.

Museveni yupo mjini London anakohudhuria mkutano wa kimataifa wa biashara na amezungumza masuala mbalimbali na BBC katika mahojiano mahsusi na Salim Kikeke huku pia akigusia hatua yake ya kumtimua kazi Waziri Mkuu Amama Mbabazi na kwamba ni suala la ndani ya chama chao cha NRM..