Tathmini ya WHO kuhusu Ebola

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko wa sasa wa ebola umewaua zaidi ya watu elfu nne miatano

Shirika la afya duniani leo linaongoza mkutano wa kamati yake ya dharura , kutathmini hali ya hivi karibuni kuhusiana na mlipuko wa Ebola .

Mkutano huo unafanyaika wakati ugonjwa huo ukiendelea kuenea katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo Guinea, Sierra Leone na Liberia - ingawa Senegal na Nigeria, ambazo zilikuwa na visa vichache zimetangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

Ni mara ya tatu sasa kamati ya dharura ya WHO inakutana .

Lengo la sasa ni kutathmini juhudi zilizofikiwa za kudhibiti ugonjwa huo na kuuzuia kuenea.

Image caption Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nne na miatano

Shirika la afya duniani linakabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kuchelewa kuzorota kuchukua hatua dhidi ya mlipuko huo , suala ambalo linaonyesha kuwa hakuna ishara ya kupungua kwa maradhi hayo katika nchi za Liberia, Guinea ama Sierra Leone.

Kamati hiyo itaangalia hatua zilizopo za uchunguzi wa mlipuko huo katika mipaka. Je hatua hizo zinafaa, na je yaweke masharti kamili ya kusafiri kwenye maeneo hayo ?

Kuna baadhi ya sababu ndogo za kuwa na matumaini - kwa pamoja Nigeria na Senegal zimeweza kuzuia kuenea kwa visa vya Ebola . Na awamu ya kwanza ya kinga za majaribio zinazoweza kuaminika zinatarajiwa kuwasili Geneva hii leo .

Lakini kinga kamili zilizoidhinishwa dhidi ya Ebola huenda zikapatikana miezi kadhaa ama baada ya mwaka