TZ:Upinzani waungana dhidi ya CCM

TZ:Upinzani waungana dhidi ya CCM

Nchini Tanzania vyama vinne vya upinzani vimetia saini Makubaliano kwa lengo la kupata nguvu ya pamoja ili kuking'oa madarakani Chama kinachotawala.

Makubaliano hayo yamewakutanisha viongozi na wafuasi wao ambapo walifanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mikutano Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Na kufuatia makubaliano hayo yaliyofikiwa na vyama hivyo vya upinzani, Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii Said Msonga, ameelezea athari zitakazotokana na makubaliano kama hayo siku za nyuma kushindikana.

Amezungumza na Regina Mziwanda