Zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na Boko haram waendelea kuzuiliwa Nigeria
Huwezi kusikiliza tena

BBC yazungumza na wasichana 3 wa Chibok

Takriban miezi sita imepita tangu zaidi ya wanafunzi wa kike mia mbili kutekwa na kundi la Boko Haram, kaskazini mashariki mwa Nigeria kijijini Chibok. Licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano na matumaini ya uwezekano wa kuachiliwa wanafunzi hawa, bado wanaendelea kushikiliwa.BBC imeweza kuzungumza na wasichana watatu walioweza kuwatoroka Boko Haram.