Ndoa za mapema zadumaza elimu TZ.
Huwezi kusikiliza tena

Ndoa za mapema zadumaza elimu TZ.

Kama sehemu ya mfululizo wa makala za BBC zijulikanazo wanawake mia moja,leo tunaangalia ndoa za utotoni nchini Tanzania, ambapo zinachangia sana kukwaza elimu ya watoto wa kike na kuwaweka katika hali ya madhara ya maisha, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za bianadamu - Human Rights Watch.

Shirika hilo limeorodhesha matukio mengi ya wasichana hadi umri wa miaka saba ambao wameozeshwa.

Wameishauri serikali ya Tanzania iweke umri wa mwisho kwa ndoa kwa wasichana na wavulana uwe miaka 18, kuondosha ndoa za utotoni.

Mwandishi wetu wa Tanzania, Abubakar Famau alitembelea mkoa wa Shinyanga ambako tabia hii bado inaendelezwa.