Huwezi kusikiliza tena

Vijana wajitosa kuuza Mbao Tanzania

Wilaya ya Mufindi ni kitovu cha biashara ya mbao nchini Tanzania. Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo ndani na nje ya nchi wanakwenda wilayani humo kwa ajili ya kununua mbao na kuzipeleka katika mikoa mengine.

Nguvu kazi inayotumika katika kukata miti na kupasua mbao inatoka kwa vijana. Hata hivyo, baadhi ya vijana hao wamelalamika kwamba malipo wanayoyapata ni madogo ikilinganishwa na nguvu wanazotumia, hivyo wanashindwa kutimiza baadhi ya malengo yao ya kimaisha.