Makataa ya watu 100 waliokutana na mathiriwa wa Ebola imekamilika
Huwezi kusikiliza tena

Mali kudhibiti kuenea kwa Ebola

Wiki moja ijayo itakuwa muhimu nchini Mali.

Zaidi ya watu 100 waliokutana na mtoto aliyefariki kutokana na Ebola watakuwa wamekamilisha siku 21 tangu kuwa karibu na mtoto huyo.

Ni muda ambao virusi vya ebola huchukua kabla ya dalili za ugonjwa kuonekana.

Anne Soy alitembelea jamii moja iliyotengwa jijini Bamako baada ya kutembelewa na mtoto huyo.