Huwezi kusikiliza tena

Anavyojikimu kupitia kwa plastiki Kenya

Na katika makala ya kuangazia ndoto ya Afrika kutana na Lorna Rutto mwanzilishi wa kampuni ya Ecopost inayofanya shughuli ya kubadili taka taka kuwa utajiri barani Afrika.

Kampuni yake ipo mjini Nairobi nchini Kenya ambapo hutumia taka taka za plastiki kutengeneza bidhaa za ujenzi na hivyo kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti.

Kupenda kwake Mazingira ndio sababu iliyomsukuma kuacha kazi ya uhasibu katika benki na kuanzisha biashara hiyo. Kama anavyosema yeye mwenyewe.

Basi usikose kutazama taarifa ya kina kuhusu mradi huo wa Lorna Ruto na jinsi unavyochangia kulinda mazingira katika matangazo yetu ya Televisheni Dira ya dunia.