Huwezi kusikiliza tena

Ebola:Hofu ya waisilamu kuhusu maziko

Na katika hatua nyingine baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wamekuwa na mashaka iwapo wapendwa wao wanaofariki kwa Ebola kama wanazikwa kwa taratibu zinazostahili.

Hii ni kufuatia maziko ya wagonjwa wa Ebola hufanyika kwa dharura ambapo watu hawaruhusiwi kukusanyika kuomboleza na hata nafasi ya kuzika ndugu zao waliokufa, isipokuwa kwa watu maalum ambapo wanaruhusiwa kuzika kutokana na kanuni za kiafya.

Na katika kujadili hili Baruan Muhuza amezungumza na Sheikh Ahmada Mbugitta wa mjini Dar es Salama na kwanza alimuuliza mambo muhumu yanayotakiwa kwa maziko ya mwislam