Huwezi kusikiliza tena

TZ yakana mpango wa kuwatimua wamasai

Serikali ya Tanzania imekanusha vikali taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa kuwa ina mpango wa kuwaondoa wamasai wapatao 40,000 katika eneo lao la urithi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Awali gazeti moja la Uingereza liliripoti mpango huo wa serikali ya Tanzania ambayo pia inadaiwa eneo hilo baada ya kuondolewa wamasi, itapewa famillia ya kifalme ya Dubai kwa ajili ya shughuli za uiwandaji.

Mwandishi wa BBC John Solombi ambaye kwa sasa yupo Dodoma amemuuliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa nchi hiyo Lazaro Nyalandu kuhusu ukweli wa taarifa hizo.