Huwezi kusikiliza tena

Mjadala kuhusu mavazi.Ni kipi sawa?

Je, wanawake wana haki kuhusu mavazi yao? Lakini ni vipi kuhusu wanaume?

Na je, kuna haja ya kuweka sheria kudhibiti mavazi ya watu? Haya ni baadhi ya maswali kwa jamii ya Afrika Mashariki na pengine Afrika kwa ujumla kwa kuzingatia mila na desturi zao.

Katika baadhi ya maeneo na kwa nyakati fulani wanawake Jijini Dar-Es-Salaam Tanzania husindikizwa kwa miluzi, mayowe, na hata kushikwa shikwa na kuchaniwa nguo pale wanapo vaa nguo zenye kuonesha ama kubana maumbile yao na kujitokeza kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi.

Mwandishi wetu REGINA MZIWANDA aliingia mitaani jijini humo na kuzungumza na baadhi ya watu ili kupata maoni yao katika suala hilo...