mashambulizi mandera
Huwezi kusikiliza tena

Al Shabaab lakiri kufanya shambulizi

Polisi nchini Kenya wanasema kuwa wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa kundi la Al Shabaab wamewauwa kwa kuwapiga risasi zaidi ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja karibu na mpaka wa Somalia.

Maafisa wa ngazi za juu wamesema kuwa basi hilo lilitekwa nyara katika Jimbo la Mandera wakati likiwa njiani kuelekea katika mji mkuu Nairobi.

Watu wasiokuwa waislamu wanasemakana kutengwa na abiria wengine na kisha kupigwa risasi.

Ifuatayo ni taarifa ya Bashkash Jugsoday