Huwezi kusikiliza tena

Utamaduni unaowaadhibu watoto Kenya

Katika kabila la Wabukusu Magharibi mwa Kenya mtu kufanya ngono na jamaa yake wa karibu ni mwiko mkubwa. Na adhabu yake ni kifo.

Lakini hata hivyo anayekumbwa na adhabu hiyo kwa sababu ya watu wawili wa karibu kushiriki ngono ni mtoto anayezaliwa.

Miezi miwili tu iliyopita baraza la Wazee kutoka kijiji kimoja katika kaunti ya Bungoma lilimhukumu adhabu hiyo ya kifo mtoto mchanga mwenye umri wa siku tatu.

Lakini kwa bahati ya mtoto huyo maafisa wa usalama na wanachama wa mashirika yasiyo ya Kiserikali walipewa taarifa na kuwahi kumwokoa mtoto huyo wa kiume.

Muliro Telewa alitembelea kaunti ya Bungoma kudadisi zaidi kuhusu utamaduni huu wa mauaji. Na hii ni taarifa yake.