Huwezi kusikiliza tena

Awashitaki madaktari kwa kumpa ARV'S kimakosa

Mwanaume mmoja nchini Kenya amewashtaki katika mahakama kuu madaktari watano wa hospitali kuu Kenyatta kwa kumpima na kusema kuwa ana Virusi vya HIV halikadhalika kumpa dawa za kupambana na makali ya virusi vya ukimwi yaani ARV.

Peter Mungai anadai kuwa alitumia dawa hizo kwa miaka mitano na zimemsababishia mwili wake kupooza.

Anadai kuwa alienda katika hospitali nyingine na alipopimwa iligundulika kuwa hana virusi hivyo.

Mwandishi wa BBC Paul Nabiswa alizungumza na wakili wake Oduor Henry kwa njia ya simu.