Loliondo
Huwezi kusikiliza tena

Polisi wadaiwa kuvuruga mkutano Loliondo

Jeshi la polisi nchini Tanzania linatuhumiwa kuusambaratisha mkutano wa amani wa hadhara uliopangwa kufanywa leo na wakaazi wa Loliondo jamii ya Wamasai Wilayani Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania.

Mkutano huo ulilenga kujadili kuhusu haki ya ardhi ya jamii hiyo ya wamasai, wanaodai serikali inataka kuwapora.

Halima Nyanza amezungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali kuhusiana na hatua hiyo ya polisi.