Huwezi kusikiliza tena

Vifo kutokana na Malaria vimepungua

Shirika la afya duniani, linasema viwango vya vifo kutokana na ugonjwa wa Malaria vimepungua tangua kuanza kwa karne ya 21.

Ripoti hiyo inaashiria jitihada ya kimataifa iliyoongezeka imesaidia kuokoa zaidi ya maisha milioni nne, wengi wao wakiwa ni watoto wa Kiafrika wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Fedha zaidi zilizotengewa ununuzi wa neti zilizotibiwa kwa dawa, utafiti wa haraka na uwepo na madawa ya kutibu yote yamechangia kupungua kwa ukubwa kwa ugonjwa huu.