Huwezi kusikiliza tena

Vita dhidi ya mauaji ya Albino TZ

Kampeni kubwa imezinduliwa Tanzania, iliyoongozwa na rais wa nchi hiyo Jakaya Kikwete, kuchangisha pesa kuwalinda albino.

Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hii imeshuhudia kuongezeka mauaji ya albino kwa imani kuwa baadhi ya sehemu zao za mwili zinaweza kuwatajirisha.

Fedha zitakazopatikana katika kampeni hiyo zitatumika kuwaelimisha watu katika jamii mbalimbali kuhusu albino. Salim Kikeke anaripoti kutoka Mwnaza, kaskazini- magharibi mwa Tanzania.