Huwezi kusikiliza tena

Kizaazaa bungeni nchini Kenya

Kulikuwa na kizaazaa kwenye bunge la Kenya siku ya Alhamisi baada ya wabunge wa upinzani kuvuruga kikao maalum kilichoitishwa kujadili mswada mpya wenye utata kuhusu usalama.

Muswada huo hatimaye umepitishwa saa chache zilizopita.

Serikali ya nchi hiyo inasema taratibu hizo zilizopitishwa zinatakiwa kupambana na wapiganaji wa al-Shabab. Lakini wapinzani wanasema taratibu hizo zitakiuka haki za binadamu.

Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza alishuhudia kitahanani.