Huwezi kusikiliza tena

Wanachuo wakosa mikopo TZ

Wanachuo zaidi ya elfu ishirini nchini Tanzania wamekosa mikopo ya elimu kutoka bodi ya mikopo nchini humo kutokana na ufinyu wa bajeti serikali huku wale wasio chukua masomo ya sayansi wengi wao ndiyo waliokosa.

Hata hivyo kila mwaka wanachuo wa chuo kikuu nchini humo wengi wao wamekuwa wakikosa mikopo hiyo kwa madai kuwa serikali haiwezi kuwalipia wote.

Baadhi ya wasomi na wanaharakati wa masuala ya kielimu wanakosoa serikali kushindwa kuwakopesha wanafunzi wote na kudai kuwa hayo ni matokeo ya maandalizi duni kufuatia ongezeko la sekondari nchini humo.

Kutoka Dar Es Salaam Leonard Mubali ametuandalia taarifa ifuatayo