Huwezi kusikiliza tena

Google yamtuza kikongwe wa Kenya

Mwanamume ajuza ambaye ametajwa katika kumbukumbu ya dunia ya Guiness kama mwanafunzi mzee zaidi, sasa amepewa tuzo na kampuni ya mtandao ya Google.

Google imeunda kikaragosi katika ukurasa wake wa juu kwa mithili ya marehemu Kimani Maruge ambaye aligonga vichwa vya habari alipojiunga na shule ya msingi akiwa na miaka 84.

Huu ni mwaka wa kumi na moja tangu tukio hilo ambapo Maruge alitaka kutumia fursa ya elimu ya bure kwa wote iliotangazwa na serikali ya Kenya

Mwandishi wa BBC Wanyama wa Chebusiri anaarifu