Benki yafunga huduma zake Somalia
Huwezi kusikiliza tena

Benki ya Marekani yafunga huduma Somalia

Benki moja nchini Marekani inayoshughulikia asilimia themanini ya fedha zinazotumwa nchini Somalia itafunga huduma yake Ijumaa, baada ya tuhuma kuibuka kuwa huenda pesa hizo zinawafikia waasi wa kundi la kiislamu la Al-Shabaab.

Fedha hizo zinazotumwa kutoka Marekani kupitia Benki ya Merchants ya California zinawapa fursa Wasomali wanaoishi nchini Marekani kutuma zaidi ya dola milioni mia mbili kila mwaka kwa jamaa zao nchini Somalia.

Mbunge mmoja nchini Marekani amesema ni jambo la kutamausha, lakini wakuu wa Benki hiyo ya Merchants wanasema hatua hiyo inafuatia ile ya kulinda ulaghai wa kifedha.

Abdullahi Ismail ni Msomalia aliyezaliwa Marekani na anaishi katika jimbo la Carlifonia. Amesema kuwa jamii ya Wasomalia jimboni Carlifonia wametamaushwa ha hatua hiyo: