Huwezi kusikiliza tena

Messi ni bingwa wa Mafahali Kenya

Mchezo wa vita vya mafahali unaendelea kuimarika eneo la magharibi nchini Kenya.

Halaiki ya mashabiki waliohudhuria pambano la wikendi iliyopita kati ya Messi na Simba katika uwanja wa Bukhungu kaunti ya Kakamega ni ishara tosha kwamba mchezo huu unapendwa sana eneo la magharibi licha ya wanaotetea haki za wanyama kusema mchezo wenyewe ni ukatili dhidi ya wanyama.

Seneta wa kaunti ya Kakamega Bonny Khalwale anasema serikali tayari imeshaanza kuwekeza kwenye mchezo huu wa mafahali ili uwe kivutio kikubwa kwa watalii.

Fahali Messi, ambaye tunaelezwa na mzee mmoja wa sehemu ya Khayega alilishwa bangi ambayo ni marufuku nchini Kenya, alimcharaza Simba kwenye pambano la kukata na shoka lililochukua dakika 30.

Kama mafahali hao wangefanyiwa ukaguzi basi huenda Messi angepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu…….John Nene alihudhuria pigano hilo na hii hapa ripoti yake….