Je kuchangia kiungo chako cha mwili ni mwiko ?
Huwezi kusikiliza tena

Je kuchangia kiungo cha mwili ni mwiko ?

Ni nadra sana kwa nchi nyingi za kiafrika kusikia mtu anaahidi kuchangia kiungo chake cha mwili.

Hii inatokana na mila na utumaduni wa nchi nyingi za kiafrika.

Kufuatia utamaduni huo kumekuwa na tatizo la baadhi ya hosptali za magonjwa ya macho kupata watu watakaochangia sehemu ya macho yao ili kuwasaidia wenye matatizo ya kiungo hicho ,na kufanya upandikizaji wa sehemu ya jicho yaani kupandikiza sehemu ya jicho la mtu mwingine kwenye jicho la mgonjwa wa macho kuwa wa gharama kubwa.

Mwandishi wetu wa Nairobi Ann Soy ametembelea hosptali moja ya macho nchi Kenya na kutuandalia taarifa ifuatayo.