Huwezi kusikiliza tena

Je unawalinda watoto na mtandao?

Dunia inaadhimisha siku ya ya matumizi ya intaneti ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni kubuni kwa pamoja intaneti bora na salama , kwa kuwaajibisha zaidi watumiaji wa intaneti hasa kupitia simu za mkononi.

Wakati simu za mkononi zenye huduma ya intaneti zikizidi kuongeza kila kukicha, ikiwa matokeo ya maendeleo teknolojia ya kisasa duniani, tishio kubwa kwa sasa ni athari za kimaadili kwa watoto pamoja na vijana wadogo ambao baadhi yao ni miongoni mwa wanaotumia simu za mkononi zenye huduma ya internet.

Muandishi wetu wa Bujumbura Ramadhani KIBUGA ametathini athari matumizi za mkononi zenye internet kwa watoto na kutuandalia taarifa ifuatayo.