Huwezi kusikiliza tena

Burundi yawaonya waandamanaji

Serikali ya Burundi imewaonya watakaofanya maandamano nchini humo watachukuliwa hatua kama wachochezi.

Akijibu wito wa mashirika ya kiraia zaidi ya mia tatu yanayotaka Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo asigombee nafasi yake hiyo kwa muhula wa tatu.

Msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo, Willy Nyamitwe amesema iwapo Rais NKurunziza atateuliwa na chama chake, na ikiwa katiba itaruhusu, basi atagombea nafasi hiyo.

Upinzani unasema muhula wa tatu wa Nkurunziza ni kinyume cha katiba na makubaliano ya Arusha na vitisho hivyo havina msingi.

Mwandishi wa BBC Ramadhan Kibuga wa amezungumza na kiongozi mkuu wa upinzani Agathon Rwasa kutoka chama cha FNL.